HUDUMA YA REDIO SAFINA YAANDAA MAALUMU YA UKOMBOZI YA KUFUNGUA MILANGO YA MIGUU.


ARUSHA.

Imeelezwa kuwa milango ya miguu ya mtu inaweza kufungwa kupitia viapo mbalimbali vinavyowekwa na wakuu wa makabila pamoja na ukoo nakumfanya mtu kushindwa kufanya jambo lolote la msingi kutokana na kuwekewa mipaka kiroho na kiuchumi.

Huduma ya redio safina kesho katika ukumbi wa maombi uliopo mbauda jijini Arusha kuanzia saa mbili hadi saa sita mchana imekuandalia maombi maalumu ya ukombozi wa kufungua milango ya miguu katika ulimwengu wa kiroho ili watu wawekwe huru mbali na viapo vinavyowatesa.

Image result for kufungua milango ya miguu
Ukombozi wa kufungua milango ya miguu katika ulimwengu wa kiroho ili watu wawekwe huru mbali na viapo vinavyowatesa.

Aidha milango ya miguu ya mtu inapofungwa na viapo vya ukoo au kabila lake hushindwa kutambua majira na nyakati sahihi za kusoma kufanya biashara,kilimo,kufuga au kufanya uvuvi kutokana na ufahamu wake kutekwa na kutumikishwa kinyume na kusudi la Mungu.
Kwa mujibu wa somo hilo la kufungua milango iliyofungwa kwa viapo vya wakuu wa makabila pamoja na ukoo watu wengi wamewekewa mipaka katika eneo la kuoa au kuolewa kupangiwa idadi ya watoto katika ndoa kupatwa na magonjwa ya kurithi, kufilisika na mara nyingine mtu kupoteza maisha.

Hata hivyo siku ya kesho katika ukumbi wa maombi uliopo mbauda  jijini Arusha kutafanyika kitendo cha imani cha kuchovya miguu kwenye mafuta ili kutakaswa na kufunguliwa milango ya miguu katika ulimwengu wa kiroho ili kufanikiwa.


HUDUMA YA REDIO SAFINA YAANDAA MAALUMU YA UKOMBOZI YA KUFUNGUA MILANGO YA MIGUU. HUDUMA YA REDIO SAFINA YAANDAA MAALUMU YA UKOMBOZI YA KUFUNGUA MILANGO YA MIGUU. Reviewed by safina radio on March 16, 2018 Rating: 5

No comments