RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI WAWILI


Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh John Magufuli leo amewaapisha mabalozi wawili ambao watawakilisha Tanzania katika nchi za Rwanda na Urusi.


Image result for PICHA YA RAIS MAGUFULI AKIMWAPISHA ERNEST MANGU KUWA BALOZI
RAIS MAGUFULI KUSHOTO AKIMWAPISHA ERNEST MANGU

Mabalozi hao walioapishwa Ikulu jijini Dar-es-salaam ni Inspekta Jenerali mstaafu wa jeshi la polisi Ernest Mangu ambaye anakwenda kuwa balozi wa Tanzania nchini Rwanda na Meja Jenerali mstaafu Saimon Marko ambaye anakuwa balozi wa Tanzania nchini Urusi.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa kwa mabalozi hao makamu wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan amewataka mabalozi hao kwenda kuwakilisha nchi vizuri katika mataifa wanayokwenda kwa manufaa ya nchi zote.

Kwa upande wake naibu waziri wa mambo ya nje,Afrika Mashariki kikanda na kimataifa Mh Suzan Kolimba amesema kuwa wizara yake iko tayari kuwapa ushirikiano mabalozi hao ili wakafanye kazi zao vizuri katika nchi walizoteuliwa kwa kujali uzalendo,uaminifu na weledi.

Naye balozi wa Tanzania nchini Rwanda IGP mstaafu Ernest Mangu amesema kuwa atatumia nguvu na akili zake zote katika kutekeleza majukumu yake ya kibalozi ambaye ameainishwa kwenye sheria na taratibu mbalimbali za nchi.

Hata hivyo hafla ya kuapishwa kwa mabalozi hao zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo katibu mkuu kiongozi Balozi John Kijazi,watendaji wa serikali na wakuu wa ulinzi na usalama.

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI WAWILI RAIS MAGUFULI AWAAPISHA  MABALOZI WAWILI Reviewed by safina radio on March 21, 2018 Rating: 5

No comments