JAMII IMETAKIWA KUFAHAMU KUWA KUNA UWEZEKANO MKUBWA WA KUVUNJA VIAPO VYA ROHO YA MAUTI KWA NJIA YA MAOMBI YA KUFUNGA PAMOJA NA KUTUMIA DAMU YA YESU KWA IMANI.


ARUSHA


Jamii imetakiwa kufahamu kuwa kuna uwezakano mkubwa wa kuvunja viapo vya roho ya mauti kwa njia ya maombi ya kufunga pamoja na kutumia damu ya yesu kwa imani.



Huduma ya redio safina Siku ya kesho katika ukumbi wa maombi uliopo mbauda hapa jijini Arusha kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa sita mchana imekuandalia maombi ya kuhitimisha somo la kuvunja viapo vya mauti ndani ya jamii.


Kwa mujibu wa somo hilo kiapo cha mauti kinaweza kukaa katika biashara,elimu,kilimo na ufugaji,pamoja na afya,huku wengine wakikabiliwa  na migogoro ya ndoa ugumu wa maisha, kufilisika au uchumi kuyumba.

Aidha pamoja na viapo hivyo vya mauti kuleta madhara makubwa ndani ya jamii imebainika kuwa damu ya Yesu ina uwezo wa kuondoa viapo hivyo ikiwa watu wataitumia damu hiyo ipasavyo kwa imani na kuomba kwa bidii.

Hata hivyo katika maombi haya ya kuhitimisha somo la kuvunja viapo vya mauti watu watafundishwa namna ya kutumia damu ya Yesu kwa imani kuvunja viapo hivyo ambapo pia watu wataombewa ili waweze kufunguliwa kwenye vifungo mbalimbali vinavyowatesa yakiwemo magonjwa sugu,laana,migogoro ya ndoa,pamoja na tatizo la ukosefu wa ajira.



JAMII IMETAKIWA KUFAHAMU KUWA KUNA UWEZEKANO MKUBWA WA KUVUNJA VIAPO VYA ROHO YA MAUTI KWA NJIA YA MAOMBI YA KUFUNGA PAMOJA NA KUTUMIA DAMU YA YESU KWA IMANI. JAMII IMETAKIWA KUFAHAMU KUWA KUNA UWEZEKANO MKUBWA WA KUVUNJA VIAPO VYA ROHO YA MAUTI KWA NJIA YA MAOMBI YA KUFUNGA PAMOJA NA KUTUMIA DAMU YA YESU KWA IMANI. Reviewed by safina radio on February 16, 2018 Rating: 5

No comments