NAIBU WAZIRI WA HABARI, JULIANA SHONZA AWATAKA WAANDISHI KUZINGATIA MISINGI KATIKA UTOAJI TAARIFA NA UCHAPISHAJI HABARI.
DODOMA.
Taarifa ya Habari saa 08:00 usiku, 13 February, 2018.
![]() |
Mh Juliana Shonza Naibu waziri wa habari utamaduni sanaa michezo. |
Naibu waziri wa habari utamaduni sanaa
michezo Mh Juliana Shonza amewataka waandishi wa habari hapa nchini kuacha
kujiingiza katika masuala ya siasa na badala yake wazingate msingi katika
utoaji wa taarifa na upashanaji habari kwa mujibu wa sheria ya huduma ya vyombo
vya habari.
Mh Shonza ameyasema hayo mjini Dodoma
alipokutana na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni siku ya
maadhimisho ya redio duniani ambapo kitaifa yamefanyika huko mkoani Dodoma.
Naibu waziri huyo ameeleza kuwa vyombo vya habari
ni mhimili mkuu unaotegemewa kufikisha elimu katika jamii hivyo havipaswi
kujiingiza katika upande wowote wa siasa.
Aidha, amesema kuwa baadhi ya waandishi wa
habari kutokuzingatia lugha fasaha ya Kiswahili na kuchanganya baadhi ya maneno
ya kigeni imekuwa ni tatizo linalosababisha jamii hapa nchini kutokupata habari
zinazoweza kuwasaidia kujiendeleza kimaendeleo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk.
Bilinith Mahenge kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari amesisitiza waandishi
kutumia kalamu na uweledi wao kuitangaza Dodoma na fursa zinazopatikana hapa
nchini.
NAIBU WAZIRI WA HABARI, JULIANA SHONZA AWATAKA WAANDISHI KUZINGATIA MISINGI KATIKA UTOAJI TAARIFA NA UCHAPISHAJI HABARI.
Reviewed by safina radio
on
February 13, 2018
Rating:

No comments