KIONGOZI WA KOREA KASKAZINI KIM JONG UN AISIFU KOREA KUSINI.

TAREHE 13-02-2017


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ameisifu Korea Kusini kwa jitihada zake nzuri za kuukaribisha ujumbe kutoka Kaskazini wakati wa mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi.

Matamshi yake yanakuja huku ujumbe, ulioongozwa na dada yake Kim Yo-jong ukirejea nyumbani kutoka Pyeongchang.
Shirika la habari la serikali KCNA lilisema kuwa Bw Kim aliishukuru Korea Kusini kwa kuupigia debe uwepo wake katika mbio hizo.

Kuhudhuria kwa Korea Kaskazini kumekuwa kwa mchango mkubwa kwa uhusiani kati ya nchi hizo.

Bi Kim na mkuu wa nchi asiye na madarakani Kim Yong-nam waliakuwa miongoni mwa maafisa wakuu waliokuwa kwenye ujumbe wa Korea Kaskazini kuzuru Korea Kusini tangu vita vya Korea Kaskazini miaka ya 1950.

Sikua ya Jumamosi Kim alimualika rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, kuzuru Pyongyang kwa mazungumzo. Ikiwa mkutano huo utafanyika utakuw wa kwanza kwa zaidi ya muongo mmoja kati ya viongozi wa Korea mbili.


KIONGOZI WA KOREA KASKAZINI KIM JONG UN AISIFU KOREA KUSINI. KIONGOZI WA KOREA KASKAZINI KIM JONG UN AISIFU KOREA KUSINI. Reviewed by safina radio on February 13, 2018 Rating: 5

No comments