WATU 20 WAMEFARIKI NCHINI INDIA


 Watu wasiopungua 20 wamepoteza maisha katika eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India kufuatia mapigano makali baina ya wanajeshi wa India na wanamgambo wanaopigania kujitenga eneo hilo linalozozaniwa la Himalaya.
Katika oparesheni dhidi ya wanaopigania kujitenga zilizoanza Jumamosi usiku, wanamgambo wasiopungua 13 wameuawa. Image result for PICHA YA ASKARI WAKIPAMBANA NA WANAMGAMBO KATIKA ENEO LA KASHMIR NCHINI INDIA
Aidha Jeshi la India limesema wanajeshi wake watatu wameuawa huku raia wanne nao wakipoteza maisha katika mapigano hayo.
Maandamano makubwa yameripotiwa Kashmir hasa katika mji wa Srinigar ambapo makundi yanaopigania kujitenga yameitisha mgomo leo Jumatatu
Kashmir ni jimbo lenye Waislamu wengi India na limekuwa likikumbwa na mzozo tokea India ipate uhuru kutoka Uingereza mwaka 1947.
Eneo lingine la Kashmir liko Pakistan ambayo pia ilikuwa koloni la Uingereza. Wakazi wa Kashmir wanataka kujitenga na India na kutangza dola lao huru au kujiunga na Pakistan.

WATU 20 WAMEFARIKI NCHINI INDIA WATU 20 WAMEFARIKI NCHINI INDIA Reviewed by safina radio on April 02, 2018 Rating: 5

No comments