WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AMETOA MAAGIZO KWA WAGANGA WAKUU WA WILAYA NA MIKOA NCHINI.
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewaagiza
waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya Nchini kuhakikisha kuwa wasimasamizi wote wa vituo
vya afya na zahanati wanaandika orodha ya dawa na vipimo vinavyopaswa kutolewa
bure na kubandika katika ubao wa matangazo.
WAZIRI WA AFYA MH. UMMY MWALIMU. |
Waziri
Ummy ametoa maagizo hayo Mkoani Kigoma wakati wa kugawa vyandarua kwa wamama
Wajawazito katika Kituo cha Afya cha Mwandiga.=
Mh.
Ummy amewataka wasimazi wa vituo vya afya vya serikali waandike katika mbao za
matangazo kuwa kipimo cha malaria, dawa mseto na sindano ya malaria kali ni
bure na hakuna malipo yoyote mgonjwa anatakiwa kulipa.
Hata
Hivyo, Zoezi hilo la ugawaji wa vyandarua vimeenda sambamba na maonyesho ya utolewaji
wa huduma za matibabu ugonjwa wa malaria kwa wananchi.
WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AMETOA MAAGIZO KWA WAGANGA WAKUU WA WILAYA NA MIKOA NCHINI.
Reviewed by safina radio
on
April 25, 2018
Rating:
No comments