ASKARI NA MAAFISA WA JWTZ WANAOSHIRIKI ZOEZI LA ULINZI NCHINI SUDANI WATUNUKIWA NISHANI NA UMOJA WA MATAIFA.
Askari na Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania
JWTZ wanaoshiriki ulinzi wa amanai nchini Sudani wametunukiwa nishani ya Umoja
wa Mataifa na kutakiwa kulinda sifa na heshima nzuri la jeshi hilo kitaifa na
kimataifa.
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Amani katika Jimbo la
Dafur Luten Jeneral Leonard Ngondi amesema kuwa Nisahini hizo ni ishara ya
mafanikio ya kazi nzuri iliyofanywa na majeshi kutoka Tanzania.
Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni wa kundi kazi
katika safu za milima ya Jabar Mara, Lameki Kawite amesema kuwa kilichooneshwa
na wanajeshi hao wakati wa utumishi na maonesho wakati wa sherehe ni ishara
tosha kuwa jeshi la Tanzania liko imara.
Hata hivyo katika kipindi chote cha uwajibikaji JWTZ
imefanikiwa kufika katika maeneo ambayo hayakuwahi kufikiwa licha ya
chanagamoto za miundombinu ambapo kwa sasa imejumuishwa katika kikosi kazi
maalumu kitakachofanya kazi katika safu za milima ya Jabar Mara ambayo hukaliwa
na waasi.
ASKARI NA MAAFISA WA JWTZ WANAOSHIRIKI ZOEZI LA ULINZI NCHINI SUDANI WATUNUKIWA NISHANI NA UMOJA WA MATAIFA.
Reviewed by safina radio
on
April 19, 2018
Rating:
No comments