WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA BIDHAA ZA SOKO LA NDANI.
Naibu waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Mh
Stella Manyanya amewataka watanzainia kutumia bidhaa za soko la ndani ikiwemo
zao la mbaazi kuliko kutegemea watu wa njee kutumia bidhaa hizo.
MH. MANYANYA |
Mh Manyanya ametoa ushauri huo leo bungeni mjini
Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Mtama Mh Nape Nnawiye
aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kutafuta soko la zao la mbaazi
ambalo kwa kiasi kikubwa limeshuka bei kutokana na kukosekana kwa soko la
uhakika.
Amesema kuwa hapo awali serikali ilikuwa inategemea
soko la mbaazi kutoka nchini India lakini baada ya India kujitosheleza na
bidhaa hiyo zao la mbaazi lilikosa soko hali iliyosababisha kushuka bei kutoka
shilingi elfu mbili kwa kilo hadi shilingi mia moja na hamsini msimu uliopita.
Ameongeza kuwa wakati huu ambapo serikali inaendelea
kutafuta soko wananchi wanatakiwa kununua na kutumia bidhaa hiyo kwani kwa sasa
bidhaa hiyo imeanza kupanda,ambapo katika masoko mbalimbali ya mkoa wa Dodoma mbaazi
inauzwa Zaidi ya shilingi elfu moja kwa kilo huku katika Supermarket za mkoa wa
Dar-es-Salaam ikiuzwa kwa Zaidi ya shilingi elfu mbili.
Hata hivyo bunge la bajeti linaendelea mjini Dodoma
ambapo wabunge wanaendelea kujadili bajeti ya ofisi ya makamu wa rais muungano
na mazingira kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 iliyowasilishwa hapo jana na
waziri wa ofisi hiyo Mh January Mkamba.
WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA BIDHAA ZA SOKO LA NDANI.
Reviewed by safina radio
on
April 17, 2018
Rating:
No comments