Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia uhalifu wa kivita ya mjini The Hague leo itaanza kusikiliza rufaa ya Radovan Karadzic
Mahakama ya Umoja wa
Mataifa inayoshughulikia uhalifu wa kivita ya mjini The Hague leo itaanza
kusikiliza rufaa ya Radovan Karadzic aliyekuwa kiongozi wa Bosnia.
FATOU BENSOUDA MWENDESHA MASHTAKA MKUU MAHAKAMA YA ICC |
Karadzic mwenye umri
wa miaka 72 alihukumiwa mnamo mwaka 2016 adhabu ya kifungo cha miaka 40 jela
baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya halaiki ya Sirebrenica na uhalifu wa
kivita mnamo mwaka 1995.
Wakili wake Peter
Robinson anataka hukumu mpya itakayozingatia haki,ambapo pia mwendesha mashtaka
mkuu anapinga rufaa hiyo kwa sababu anaiona adhabu aliyopewa Karadzic ni ndogo.
Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia uhalifu wa kivita ya mjini The Hague leo itaanza kusikiliza rufaa ya Radovan Karadzic
Reviewed by safina radio
on
April 23, 2018
Rating:
No comments