BUNGE LA BURUNDI LAPITISHA SHERIA POLISI KUAGUA NYUMBA ZA RAIA BILA KIBALI MAALUMU.


Bunge nchini Burundi limepitisha mswada wa sheria uliyowasilishwa na Waziri wa Sheria, kuruhusu polisi kufanya ukaguzi katika makazi ya watu bila kibali maalum.
Image result for bunge la rwanda
Waziri wa Sheria Aimé Laurentine Kanyana aliutetea mswada huo kwa kile alichokitaja kuwa Burundi inakabiliwa na visa vya mauaji ya kikatili,ugaidi, baishara ya binadamu na kumiliki silaha kinyume cha sheria, utumiaji wa dawa za kulevya na hata ubakaji.
Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa mswada huo umepitishwa kwa kura 97 huku ukipingwa kwa kura 22 za wabunge wa upinzani, hatua ambayo  imekosolewa vikali na wapinzani na watetezi wa haki za binadamu nchini humo.
Vyama vya upinzani nchini humo, vimehofia utaratibu huo, ambapo mkuu wa chama cha upinzani, UPRONA, Abel Gashatsi ameeleza, kuwa Nchi ya Burundi imetoka katika vita, hivyo ni lazima watu waogope.
Kwa upande wa chama kikongwe cha upinzani, FRODEBU wanasema muswada huo unakiuka katiba na kupendekeza baraza la Seneti kuurejesha na kuupinga.

BUNGE LA BURUNDI LAPITISHA SHERIA POLISI KUAGUA NYUMBA ZA RAIA BILA KIBALI MAALUMU. BUNGE LA BURUNDI LAPITISHA SHERIA POLISI KUAGUA NYUMBA ZA RAIA BILA KIBALI MAALUMU. Reviewed by safina radio on April 20, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.