IDARA YA TAKWIMU KENYA YAONGELEA KIWANGO CHA KUPANDA NA KUSHUKA KWA UCHUMI WA KENYA.


Idara ya takwimu ya Kenya imesema kuwa pato la taifa la mwaka 2017 limeongezeka kwa asilimia 4.9, ambapo ni kushuka kwa asilimia moja ikilinganishwa na mwaka 2016 huku ikiwa ni kasi ndogo zaidi ya ongezeko katika miaka mitano iliyopita.

        Image result for KENYA
Ripoti iliyotolewa na idara hiyo imesema sababu kuu ya kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi nchini Kenya kwa mwaka jana ni ukosefu wa utulivu wa kisiasa na hali mbaya ya hewa iliyosababisha uhaba wa mazao ya kilimo.

Aidha ripoti hiyo pia imesema mwaka jana pato la utalii la Kenya liliongezeka kwa asilimia 20.3 ikilinganishwa na lile la mwaka 2016.

IDARA YA TAKWIMU KENYA YAONGELEA KIWANGO CHA KUPANDA NA KUSHUKA KWA UCHUMI WA KENYA. IDARA YA TAKWIMU KENYA YAONGELEA KIWANGO CHA KUPANDA NA KUSHUKA KWA UCHUMI WA KENYA. Reviewed by safina radio on April 26, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.