URUSI KUPENDEKEZA WACHUNGUZI WA KIMATAIFA


 Nchi ya leo Urusi imesema kwamba itapendekeza kwa Umoja wa Mataifa wachunguzi wa kimataifa kutembelea eneo linaloshukiwa kutokea shambulio la silaha za kemikali katika mji wa Syria, Douma kuwabaini waliohusika
Image result for PICHA YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA URUSI SERGEI LAVROV
SERGEI LAVROV

Hatua hiyo imekuja baada ya kitisho cha Rais wa Marekani Donald Trump kuichukulia hatua ya haraka za kijeshi dhidi ya serikali ya Syria baada ya shambulio hilo la kemikali kutokea.

Rais wa Syria Bashar al-Assad pamoja na Urusi ambayo ni mshirika wake wa karibu, wamesema hakuna ushahidi unaoonesha kuwa  kumefanyika shambulio la kemikali na kwamba madai hayo hayana msingi.

Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sagey Lavrov amesema kuwa mara kadhaa wamekwisha eleza kuwa Wawakilishi wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Syria na wawakilishi wa Kirusi ambao wanasimamia usalama wa redilojia wametembelea eneo linaloshukiwa kutokea tukio hilo huko Douma na hawajaona tatizo lolote la kemikali.

Hata hivyo Takriban watu 60 wameuawa na wengine zaidi ya elfu moja wamejeruhiwa katika maeneo kadhaa katika shambulio linalodaiwa kutokea katika mji wa Douma, ambao kwa wakati huo ulikuwa bado unadhibitiwa na vikosi vya waasi.

URUSI KUPENDEKEZA WACHUNGUZI WA KIMATAIFA URUSI KUPENDEKEZA WACHUNGUZI WA KIMATAIFA Reviewed by safina radio on April 11, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.