HOSPITALI YA MANISPAA YA IRINGA FRELIMO YAKABILIWA NA UKOSEFU WA VIFAA.
MAJENGO YA HOSPITALI YA MANISPAA YA IRINGA FRELIMO |
Aidha Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dk. Pilila
Zambi amesema kuwa hospitali hiyo kwa sasa inawahudumia wananchi zaidi ya laki
mbili na hivyo kuzidiwa uwezo kutokana na kukosa baadhi ya majengo muhimu ikiwemo
jengo la kuhifadhia maiti.
Kufuatia hali hiyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Bw
Omary Mkangama amesema kuwa Halmashauri ya Manispaa hiyo imetenga bajeti ya
kiasi cha fedha milioni 100 ili kutatua baadhi ya changamoto kwa awamu.
Aidha, Halmashauri hiyo ya Manispaa ya Iringa inaendelea
kuwatafuta wadau mbali mbali ili kuhakikisha kuwa changamoto zinazoikumba
hospitali hiyo zinatatuliwa.
HOSPITALI YA MANISPAA YA IRINGA FRELIMO YAKABILIWA NA UKOSEFU WA VIFAA.
Reviewed by safina radio
on
April 11, 2018
Rating:
No comments