WAKULIMA WA MANISPAA YA SONGEA MKOANI RUVUMA WAMEPATIWA MAFUNZO YA KILIMO CHA KAHAWA
Wakulima wa Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
wamepatiwa mafunzo sahihi ya kilimo cha zao la kahawa kupitia tafiti
zilizofanywa na Taasisi ya Utafiti wa zao la Kahawa Tanzania TAKRI.
Meneja wa Taasisi ya Utafiti wa zao la Kahawa
Tanzania TAKRI kutoka kituo cha Ugano kilichopo wilaya ya Mbinga Bw Godbless
Shao amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha maafisa wa kilimo wa
Manispaa hiyo kutoa elimu bora kwa wakulima.
Naye Mtaalamu wa kilimo kutoka Manispaa hiyo ya
Songea Philipina Tarimo amesema kuwa elimu waliyoipata itasaidia kuinua kipato
cha wakulima na kuboresha maisha yao.
WAKULIMA WA MANISPAA YA SONGEA MKOANI RUVUMA WAMEPATIWA MAFUNZO YA KILIMO CHA KAHAWA
Reviewed by safina radio
on
April 13, 2018
Rating:
No comments