VIJANA KATI YA MIAKA 15-19 WAPO KATIKA HATARI YA MAAMBUKIZI VVU.


Kundi la Vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 19 hasa wa kike limetajwa kuwa ndilo kundi kubwa zaidi lililopo kwenye hatari ya maambukizi ya virusi vya ukimwi  na linapaswa kupewa kipaumbele cha uelewa katika kujikinga na maambukizi hayo.

Hayo yamesemwa na mtaalamu wa virusi vya UKIMWI kutoka shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF ofisi ya Dar es salaam Dk. Sajida Kimambo wakati wa kuwasilisha matokeo ya viashiria vya UKIMWI katika mkoa wa Songwe na kutoa rai kwa vijana kujitokeza ili kufahamu mapema hali ya afya zao.


Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dk. Herri Kagya amesema kuwa takwimu hizo ni muhimu kwa mkoa huo.

Mkuu wa Wilaya ya Momba Juma Milando amesema kuwa wakati huu wafadhili wa miradi ya UKIMWI wameanza kupunguza misaada kwa serikali hivyo Halmashauri za Wilaya ni lazima zitenge bajeti inayotekelezeka kwa ajili ya shughuli zinazolenga kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Hata hivyo, Bw. Milando ameyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe wakati wa kupokea taarifa hiyo ya matokeo ya viashiria vya UKIMWI.

VIJANA KATI YA MIAKA 15-19 WAPO KATIKA HATARI YA MAAMBUKIZI VVU. VIJANA KATI YA MIAKA 15-19 WAPO KATIKA HATARI YA MAAMBUKIZI VVU. Reviewed by safina radio on April 30, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.