SERIKALI KUENDELEA KUPUNGUZA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOZIKABILI SHULE ZA SEKONDARI NCHINI.
Naibu waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa
na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh
Joseph Kakunda amesema kuwa serikali itaendelea kupunguza changamoto mbalimbali
zinazokabili shule za sekondari hapa nchini ikiwemo upungufu wa waalimu wa sayansi.
NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI MH. KAKUNDA. |
Mh Kakunda ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma
wakati akijibu swali la Mh Hamidu Mobali aliyetaka kujua ni lini serikali
itamaliza tatizo la upungufu wa waalimu wa shule za sekondari hapa nchini.
Amesema kuwa mpango uliopo kwa sasa ni serikali
kuwaajiri walimu wa sayansi wapatao mia sita kufikia Juni 30 mwaka huu lengo
likiwa ni kuondoa kabisa tatizo la waalimu wa sayansi na hisabati katika shule
za sekondari ifikapo mwaka wa 2020.
Katika hatua nyingine Mh Kakunda amesema kuwa
serikali haijakataza michango ya wananchi ya kusaidia kujenga miundombinu ya
shule ikiwemo maabara ila serikali ilichokataza ni kumpa mwanafunzi adhabu ya
kukosa masomo kutokana na mzazi wake kutotoa michango.
Hata hivyo bunge la bajeti linaendelea mjini Dodoma
ambapo wabunge wanaendelea kujadili bajeti za wizara mbalimbali kwa mwaka wa
fedha wa 2018/2019.
SERIKALI KUENDELEA KUPUNGUZA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOZIKABILI SHULE ZA SEKONDARI NCHINI.
Reviewed by safina radio
on
April 16, 2018
Rating:
No comments