WABUNGE WATAKIWA KUCHUKUA HATUA STAHIKI KUDHIBITI UNYANYASAJI WA KIJINSIA.
Wabunge wametakiwa kuchukua hatua stahiki kudhibiti
vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vinavyofanywa dhidi ya wanawake na watoto wenye
walemavu.
Ushauri huo umetolewa kwa wabunge baada ya utafiti
uliofanywa na shirika la Action On Disabillity and Development kwa kushirikiana
na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye ulemavu kubaini kuwepo kwa baadhi ya udhalilishaji
dhidi ya wanawake na watoto wenye ulemavu.
Utafiti huo umewekwa bayana kwa wabunge ambapo
inadaiwa kuwa baadhi ya ndugu na jamaa wamekuwa wakishirikiana kufanya vitendo
vya udhalilishaji wanawake na watoto wenye ulemavu hususani wenye ulemavu wa
kusikia na akili.
Baadhi ya wabunge wamedai kuwa utaratibu wa elimu
jumuishi ni moja njia muhimu itakayoweza kupunguza matatizo ya walemavu ikiwa
shule za msingi na sekondari zitapatiwa vifaa, wataalamu na miundombinu ya
kuwezesha watu wenye ulemavu kupata elimu pamoja na wanafunzi wengine wasio na
ulemavu.
WABUNGE WATAKIWA KUCHUKUA HATUA STAHIKI KUDHIBITI UNYANYASAJI WA KIJINSIA.
Reviewed by safina radio
on
April 23, 2018
Rating:
No comments