ZANA HARAMU ZA UVUVI ZAKAMATWA MKOANI MWANZA
Operesheni Sangara awamu ya pili imefanikiwa kukamata
zana haramu za uvuvi pamoja na injini tano za boti zinazosadikika kuwa ni za
wizi zikiwa zimefukiwa ardhini kwenye eneo la nyumba ya mfanyabiashara mmoja wa
samaki mkoani Mwanza.
Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Kanerd
Katunusi amesema kuwa nyavu hizo zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni
hamsini ni miongoni mwa zana za Uvuvi ambazo zilipigwa marufuku kutokana na madhara
yake kwa viumbe vya ziwani.
Aidha Afisa Uvuvi huyo wa Halmashauri ya jiji la
Mwanza amesema kuwa zana hizo zimepatikana baada ya maafisa wa kikosi maalumu
cha kupambana na uvuvi haramu katika ziwa Victoria Wilayani Nyamagana kufukua
shimo moja kwenye ua wa nyumba ya mfanyabiashara huyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa
Mwananchi Elifance Masinde amesema kuwa zana hizo haramu zimekutwa zimefukiwa
kwenye eneo la nyumba Kondo na eneo la Mtaa wake wa Mwananchi jijini Mwanza.
Katika Operesheni hiyo kumebainika kuwa injini tano
za boti zilizokutwa kwenye shimo hilo zina thamani ya zaidi shilingi milioni
ishirini zinazosadikiwa kuwa ni za wizi huku
watu waliokutwa katika makazi ya mfanyabiashara huyo wakishikiliwa na jeshi la
polisi kwa uchunguzi zaidi.
ZANA HARAMU ZA UVUVI ZAKAMATWA MKOANI MWANZA
Reviewed by safina radio
on
April 24, 2018
Rating:
No comments