ANGELA MERKEL KUKUTANA NA TRUMP
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel atakutana leo na
Rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House, akikabiliwa na
kibarua kigumu cha kuukoa muafaka wa nyuklia wa Iran, kuepusha vita vya
kibiashara na kuyafanya mahusiano yake na rais huyo wa Marekani kuanza tena
kufanya kazi.
Ziara ya kiongozi huyo wa Ujerumani tayari imegubikwa
na mazungumzo yaliyoonekana kuwa ya undugu kati ya Donald Trump na Rais wa
Ufaransa Emmanuel Macron wiki hii.
Saa chache tu kabla ya Kansela Merkel kutua jana usiku
nchini Marekani, ikiwa ni miezi 15 baada ya Trump kuapishwa kuwa rais, Bunge la
Marekani hatimaye lilifanikiwa kumuidhinisha balozi wa nchi hiyo nchini
Ujerumani.
Hata hivyo Muda
mfupi baada ya uteuzi wake, Richard Grenell
anayejulikana kwa msimamo wake wa kihafidhina na mtetezi mkubwa wa sera
za Trump za ``Marekani Kwanza” alithibitishwa kuchukua wadhifa huo.
ANGELA MERKEL KUKUTANA NA TRUMP
Reviewed by safina radio
on
April 27, 2018
Rating:
No comments