WAAJIRI NCHINI WAMETAKIWA KUWASILISHA MAJINA YA WAFANYAKAZI BODI YA MIKOPO
Waajiri kote nchini ambao hawajawasilisha majina ya
wafanyakazi kwenye bodi ya mikopo ya
wanafunzi wa elimu ya juu kwa ajili ya uhakiki wametakiwa kufanya hivyo kabla
hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.
BW. PHIDELIS JOSEPH |
Akizungumza jijini Mwanza alipotembelea hospitali ya
Uhuru Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji Mikopo wa Bodi hiyo Bw. Fidelis Joseph
amesema kuwa baadhi ya waajiri hawajawasilisha majina ya wafanyakazi wao kwenye
bodi hiyo.
Aidha, amebainisha kuwa tatizo la watendaji
kutokutoa ushirikiano kwa watumishi wa Bodi huku akisema kuwa sheria ya bodi
hiyo inaeleza kuwa endapo mtu yeyote atawazuia watendaji hao wa bodi anaweza
kukamatwa mara moja na kupelekwa katika maeneo ya kisheria.
Wakiwa jijni humo maafisa wa bodi hiyo wametembelea
hospitali ya uhuru na shule za Allience na kubaini kuwa zaidi ya wafanyakazi
mia moja,majina yao hayajawasilishwa kwenye bodi ya mikopo kwa ajili ya kuhakikiwa.
WAAJIRI NCHINI WAMETAKIWA KUWASILISHA MAJINA YA WAFANYAKAZI BODI YA MIKOPO
Reviewed by safina radio
on
April 19, 2018
Rating:
No comments