VIONGOZI NA RAIA WA KENYA WATOA WITO KWA TUME YA UCHAGUZI KUVUNJWA.


Viongozi na raia wa Kenya wametoa wito wa kuvunja tume ya uchaguzi baada ya makamishna watatu kujiuzulu kutokana na migongano ya siasa isiyoisha.
Image result for TUME YA UCHAGUZI KENYA
Migongano hiyo imeanza mwaka jana kwenye vipindi viwili vya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo,ambapo makamishna watatu wa tume ya uchaguzi wamejiuzulu juzi nyadhifa zao za uongozi ndani ya tume hiyo.

Aidha, duru za habari zinaeleza kuwa makamishna hao waliojiuzulu nyadhifa zao za uongozi ni pamoja na Consalata Maina, Paul Kurgat na Margaret Mwachanya .

Habari zinaeleza kuwa kiwango cha imani ya wananchi dhidi ya tume hiyo kimeshuka zaidi, na inaonekeana kuwa kuvunjwa kwa tume hiyo ndio njia pekee ya kutatua suala hilo.

Hata hivyo kwa mujibu wa sheria, makamishna watano kati ya saba wa tume hiyo wanaweza kufanya maamuzi, lakini kwa vile sasa kuna ukosefu wa makamishna watatu, tume hiyo haiwezi kufanya kazi ipasavyo.

VIONGOZI NA RAIA WA KENYA WATOA WITO KWA TUME YA UCHAGUZI KUVUNJWA. VIONGOZI NA RAIA WA KENYA WATOA WITO KWA TUME YA UCHAGUZI KUVUNJWA. Reviewed by safina radio on April 18, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.