MAPADRI WAWILI WAUAWA NA WAUMINI 16 NCHINI DRC.


Mapadri wawili wa kanisa Katoliki na waumini 16 wa kanisa hilo wameuawa katika shambulizi lililotokea katika kijiji cha Mbalom katika jimbo la Benue, nchini Nigeria siku ya jana.
Image result for picha ya shambulio la kigaidi nchini nigeria
Shambulizi hilo lililotokea katikati mwa nchi ambako kumeendelea kushuhudiwa mapigano ya kikabila yanayohusisha  wafugaji waliokua wamebeba silaha,ambapo washambuliaji hao waliingia katika kanisa wakati wa sherehe ya mazishi katika kijiji cha Mbalom, katika jimbo la Benue, nchini Nigeria.
Mapadri wawili na waumini 16 wa kanisa Katoliki, wote waliuawa kwa kupigwa risasi, kwa mujibu wa mashahidi walionukuliwa na shirika la habari la AFP ambao pia wamesema watu wengi walijeruhiwa.
Dayosisi ya Makurdi, mji mkuu wa Jimbo la Benue, imelaani vurugu ambazo zilikumba mojawapo ya makanisa yake huku  Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo akiahidi kuwaadhibu wale wote waliohusika na katika tukio hilo kwa mujibu wa sheria.

MAPADRI WAWILI WAUAWA NA WAUMINI 16 NCHINI DRC. MAPADRI WAWILI WAUAWA NA WAUMINI 16 NCHINI DRC. Reviewed by safina radio on April 25, 2018 Rating: 5

No comments