HUDUMA YA REDIO SAFINA IMEANDAA MAFUNDISHO NA MAOMBI KWA AJILI YA KUTAMBUA KUSUDI LA MUNGU NDANI YA MTU.
Imebainishwa kuwa baadhi ya watu wameshinda kutambua
kusudi la Mungu lililoko ndani yao jambo ambalo linawafanya waendelee kuishi
maisha duni kutokana na kushindwa kumudu kazi zao kama vile biashara,Afya,kilimo,ufugaji
na huduma kwa ujumla.
Huduma ya redio safina kesho katika ukumbi wa maombi
uliopo mbauda jijini Arusha kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa saba mchana imekuandalia mafundisho na maombi maalum
kuhusu namna ya kutambua kusudi lililowekwa na Mungu ndani ya mtu.
Kutokana na watu wengi kushindwa kutambua kusudi la
Mungu waliloliwekewa ndani yao wamejikuta wakikumbana na
matatizo mbalimbali ikiwemo magonjwa,kuporomoka kwa uchumi,kukosa kazi,kutokuoa
au kuolewa huku wengine wakikosa watoto na mara nyingine mimba kuharibika.
Sambamba na hayo kesho kutafanyika maombi maalum ya kufufua
vipawa na karama kama vile huduma,biashara kilimo ufugaji, vyote ambavyo
vilikuwa vimeshikiliwa na adui kwa muda mrefu na kusababisha Baraka kutokufikia
watu kwa wakati.
Hali
kadhalika kesho watu wenye mahitaji mbalimbali wataombewa ili kufunguliwa dhidi
magonjwa,madeni na nguvu za giza.
HUDUMA YA REDIO SAFINA IMEANDAA MAFUNDISHO NA MAOMBI KWA AJILI YA KUTAMBUA KUSUDI LA MUNGU NDANI YA MTU.
Reviewed by safina radio
on
April 18, 2018
Rating:
No comments