WATU 63 WAPOTEZA MAISHA MJINI KABUL.
Watu 63 wamepoteza maisha jijini Kabul nchini Afghanistan baada
ya kutokea kwa mashambulizi ya bomu katika maeneo mbalimbali ya kujiandikisha wapiga
kura.
![]() |
MAJERUHI WAKIPATIWA MATIBABU |
Taarifa kutoka mamlaka mjini Kabul zinasema kuwa wanawake 21 na
watoto watano ni miongoni mwa waliouawa na watu 119 wamejeruhiwa katika
mashambulizi hayo.
Mlipuko huo pamoja na kusababisha vifo umeharibu magari ,ambapo hadi sasa kumekuwa na
mashambulio manne tangu kuanza uandikishaji huo wiki iliyopita.
Kundi la Islamic State limesema ndilo lililohusika na shambulizi
hilo lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hata hivyo Kazi ya uandikishaji wapiga kura nchini humo imeanza
mwezi uliopita ikiwa ni maandalizi kwaajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
WATU 63 WAPOTEZA MAISHA MJINI KABUL.
Reviewed by safina radio
on
April 23, 2018
Rating:
No comments