UFARANSA KULIPIZA KISASI


Ufaransa imesema italipiza kisasi dhidi ya utawala wa Syria wa Rais Bashar al-Assad iwapo kutatokeza ushahidi kwamba ulihusika na kile kinachoshukiwa kuwa ni shambulio la gesi ya sumu ya klorini katika eneo linalodhibitiwa na waasi.
Image result for PICHA YA EMMANUEL MACRON WA UFARANSA
EMANUEL MACRON
Aidha, Msemaji wa serikali ya Ufaransa Benjamin Griveauksi ameiambia Redio Europe nambari moja, kwamba taarifa za upelelezi za Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na Donald Trump wa Marekani zinaashiria silaha za kemikali zilitumika.

Hata hivyo, Viongozi hao wawili wamezungumza kwa simu jana usiku kuhusu shambulizi lililotokea kwenye mji wa Douma siku ya Jumamosi iliyopita ambapo zaidi ya watu 40 waliuawa katika kile kinachotajwa kuwa ni shambulio la gesi ya sumu.

UFARANSA KULIPIZA KISASI UFARANSA KULIPIZA KISASI Reviewed by safina radio on April 11, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.