AMISOM YAITAKA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUISADIA SOMALIA
Tume
ya Umoja wa Afrika ya Kulinda Amani nchini Somalia AMISOM imeitaka jumuiya ya
kimataifa kusaidia Somalia kuijengea uwezo wa kukabiliana na vitisho nchini
humo.
Wakihitimisha
mkutano wa nne wa mwaka, Maafisa wakuu wa AMISOM wakiwemo maafisa wa usalama
wamefikia makubaliano juu ya hatua za kukabiliana kwa ufanisi na tishio la
mabomu ya kienyeji linalozuia mchakato wa kupata utulivu nchini humo.
Mwakilishi
maalum wa mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia Francisco
Madeira, amewapongeza washirika mbalimbali kwa kuendelea kuwaunga mkono na
kujitolea askari wake kwa AMISOM kukabiliana na tishio la mabomu ya kienyeji
(IED) kwa vikosi vya usalama na raia wa Somalia.
Mapema
mwezi huu Kitengo cha Huduma za kutegua Mabomu cha Umoja wa Mataifa kimesema kuwa
takriban watu 3,000 wanasadikika kuuawa na kujeruhiwa kutokana na mabomu hayo
nchini Somalia.
AMISOM YAITAKA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUISADIA SOMALIA
Reviewed by safina radio
on
April 19, 2018
Rating:
No comments