MAHAKIMU 250 WAFUTWA KAZI NCHINI DRC
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
imewafuta kazi Mahakimu 250 ambao hawana elimu ya sheria pamoja na wale ambao
walikuwa wameshtumiwa kuwa mafisadi.
Waziri wa Sheria wa nchi hiyo Alexis Thambwe Mwamba
amesema hatua hii imechukuliwa ili kuwazuia watu waliokuwa wanaingia katika
idara ya Mahakama wakiwa na lengo la kujipatia fedha badala ya kuwatumikia raia
wa nchi hiyo.
Hii sio mara ya kwanza kwa serikali ya Kinshasa
kuwachukulia hatua maafisa wa juu wa idara ya Mahakama kwani Mwaka 2009, rais
Joseph Kabila aliwafuta kazi Majaji 96 baada ya kubainika kuwa walikuwa mafisadi.
MAHAKIMU 250 WAFUTWA KAZI NCHINI DRC
Reviewed by safina radio
on
April 17, 2018
Rating:
No comments