TANGA KUJENGA SOKO KUBWA LA MATUNDA
Mkoa
wa Tanga umejipanga Kujenga soko la Kimataifa la matunda na mboga mboga katika
eneo la Segera Wilayani Handeni ili kuwa na uhakika wa kuuza bidhaa za
mashambani na kupata bei nzuri ya ushindani.
Hayo
yamesemwa na katibu tawala wa Mkoa huo
Bi,Anuciata Lyimo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na namna ambavyo wamejipanga kuimarisha hali ya masoko mkoani humo.
Amesema
kuwa ili wakulima wa matunda waweze kupata soko la uhakika mkoa huo unadhamiria
kujenga soko la kimataifa katika eneo la Segera ili kuwawezesha wakulima
kunufaika na bei nzuri za bidhaa wanazozizalisha wenyewe mashambani.
Pia
ameongeza kuwa ili kuhakikisha wakulima wananufaika na soko lenye tija
mkoa huo umejikita kuboresha masoko yote ya ndani kwa kuweka
miundombinu ya maji ,vyoo,umeme,na barabara ili kuhakikisha kwamba bidhaa
zinazozalishwa zinapata soko la uhakika ndani na nje ya nchi.
Aidha
Bi Lyimo ameelezea changamoto inayoikabili sekta ya masoko mkoani humo kuwa ni
kukosekana kwa soko la uhakika kwa bidhaa zinazozalishwa viwandani kutokana na
matumizi ya vifungashio duni pamoja na ukosefu wa mitaji mikubwa ya kufufua na
kuendeleza viwandwa vilivojengwa miaka ya 1980.
TANGA KUJENGA SOKO KUBWA LA MATUNDA
Reviewed by safina radio
on
April 19, 2018
Rating:
No comments