KANSELA MERKEL ASEMA SERIKALI YAKE IKO TAYARI
Kansela Angela Merkel amesema kuwa serikali yake iko
tayari kuiongoza Ujerumani, licha ya kuwepo na hali ya kurushiana maneno
miongoni mwa viongozi wa vyama vinavyounda serikali yake.
Akizungumza baada ya mkutano wa siku mbili na baraza
lake la mawaziri, Merkel amesema huenda kukawa na majibizano miongoni mwa
viongozi, lakini ni wazi kuwa ipo nia ya kufikia makubaliano kuhusu masuala ya
nchi.
Merkel alianza muhula wake wa nne, na ambao
unaonekana kuwa wa mwisho, akikabiliwa na changamoto ya kuongoza serikali ya
muungano kati ya kundi la vyama vyake vya kihafidhina vya CDU na CSU, na chama
sha SPD wakati umaarufu wake ukiendelea kupungua kufuatia mgogoro wa wakimbizi
ulioanza mwaka wa 2015 nchini Ujerumani.
KANSELA MERKEL ASEMA SERIKALI YAKE IKO TAYARI
Reviewed by safina radio
on
April 12, 2018
Rating:
No comments