WANAFUNZI WA VYUO WAMETAKIWA KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA


Wanafunzi wa vyuo mbalimbali hapa nchini wametakiwa kuwa na utaratibu wa kujiunga na bima ya afya pamoja na mali zao ili kuweka akiba pindi wanapokumbwa na majanga mbalimbali ili wafidiwe kwa kile walichokiekeza.
Image result for PICHA YA WANAFUNZI WA CHUO

Hayo yamesemwa jijini Arusha na Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini TIRA Elieza Rekiza wakati akitoa elimu ya matumizi ya bima  kwa wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA kilichopo Oljoro mkoani Arusha.
Aidha, amesema kuwa bado kuna tatizo kubwa la uelewa mdogo kwa wananchi kuhusu umuhimu wa bima hizo hivyo ni vyema elimu ikatolewa mara kwa mara ili wananchi wapate uelewa mkubwa zaidi juu ya suala hilo.
Kwa upande wake, Meneja wa kanda ya kaskazini wa Kampuni ya Zanzibar Insuarrence Cooporation Bw Mohamed Matumla amesema kuwa makundi ya vijana yaliyoko katika taasisi za elimu wanahitaji kuelimishwa na kuwa watumiaji wakubwa wa huduma ya bima.
Hata hivyo baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho cha ufundi VETA Oljoro wamesema kuwa mafunzo ya uelewa juu ya huduma za bima inasaidia kujua kiundani kuhusu shughuli za bima na namna zinavyoweza kuwasaidia.



WANAFUNZI WA VYUO WAMETAKIWA KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA WANAFUNZI WA VYUO WAMETAKIWA KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA Reviewed by safina radio on April 17, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.