MFALME WA SWAZILAND MSWATI WA TATU AMETANGAZA KUBADILISHA JINA LA NCHI HIYO.


Mfalme wa Swaziland, Mswati wa Tatu, ametangza kubadilisha jina la nchi yake ambayo sasa itajulikana kama Ufalme wa ESwatini.
Image result for PICHA YA MFALME WA SWAZILAND MSWATI WA TATU
MFALME MSWATI WA TATU
Rais huyo ametangaza uamuzi huo wa ghafla katika sherehe za mwaka wa 50 wa uhuru wa Uswazi pamoja na maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwake ambapo pia ametimiza miaka 50.
Katika mikutano kadhaa ya hadhara Mfalme Mswati wa Tatu amekuwa akiitaja nchi yake kwa jina la eSwatini, kwa maana ya 'ardhi au nchi ya Waswazi' kwa lugha ya Kiswati au Kiswazi.
Mfalme Mswati amesema mabadiliko hayo yatasababisha nchi yake irejee katika jina lake la asili kabla ya zama za ukoloni wa Muingereza,ambapo Nchi hiyo ndogo ya kusini mwa Afrika ilipata uhuru wake mwaka 1968.
Aidha mfalme huyo amesema jina hilo jipya pia litasaidia kutatuliwa kwa tatizo la kimataifa ambapo watu wengi wamekuwa wakiitaja nchi hiyo kuwa ni Switzerland, nchi ya Ulaya Magharibi.



MFALME WA SWAZILAND MSWATI WA TATU AMETANGAZA KUBADILISHA JINA LA NCHI HIYO. MFALME WA SWAZILAND MSWATI WA TATU AMETANGAZA KUBADILISHA JINA LA NCHI HIYO. Reviewed by safina radio on April 20, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.