WATU 36 WAHUKUMIWA ADHABU YA KIFO NCHINI MISRI


Mahakama ya kijeshi nchini Misri imewahukumu watu thelathini na sita adhabu ya kifo kutokana na makosa ya mashambulizi dhidi ya makanisa ya Coptic.
Image result for PICHA YA MAHAKAMA NCHINI MISRI
Watu sabini walikufa kutokana na shambulizi la bomu katika kanisa kuu la ki Coptic mjini Cairo mwishoni mwa mwaka 2016, huku makanisa ya Alexandria na Tanta yakilipuliwa siku kama hiyo mwezi wa nne mwaka uliofuata.
Tayari kundi la wanamgambo wa kiislamu wenye msimamo mkali wamekiri kuhusika na mashambulizi hayo matatu.
Pia wanamgambo hao wameendelea kukiri kuwa kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwashambulia wakristo wachache, pamoja na mamlaka ya kijeshi.

Misri inahitaji mahakama kupeleka kesi za namna hiyo kwa Mufti mkuu nchini humo kwa kuzingatia adhabu ya kifo kabla ya hukumu ya mwisho.

WATU 36 WAHUKUMIWA ADHABU YA KIFO NCHINI MISRI WATU 36 WAHUKUMIWA ADHABU YA KIFO NCHINI MISRI Reviewed by safina radio on April 11, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.