WACHUNGUZI KUZURU DOUMA HUKO SYRIA.
Urusi imesema kuwa wachunguzi wa silaha za kemikali
nchini Syria wataruhusiwa kuzuru katika eneo linalodaiwa kushambuliwa na silaha
za sumu siku ya Jumatano
Kundi hilo la kimataifa limekuwa nchini humo tangu siku
ya Jumamosi lakini halijaruhusiwa kuingia Douma.
Shambulio hilo la siku ya Aprili 7 lilifuatia
shambulio linguine dhidi ya serikali ya Syria lililotekelezwa kwa pamoja na
Marekani, Uingereza na Ufaransa wiki moja baadaye.
Syria na mshirika wake Urusi wamekana shambulio
lolote la kemikali huku Urusi ikitaja madai hayo kama 'yaliopangwa'.
Mapema siku ya Jumanne , chombo cha habari cha Syria
kilisema kuwa ulinzi wa angani wa taifa hilo ulikabiliana na shambulio la
makombora juu ya anga ya magharibi mwa mji wa Homs.
WACHUNGUZI KUZURU DOUMA HUKO SYRIA.
Reviewed by safina radio
on
April 17, 2018
Rating:
No comments