MAGUFULI AWAACHIA HURU ZAIDI YA WAFUNGWA 3000.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa wote kupunguziwa
robo ya adhabu zao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu ambapo wafungwa
hao sharti wawe wametumikia robo ya adhabu zao gerezani isipokuwa wafungwa
walioorodheshwa kwenye ibara ya pili.
Wafungwa wengine waliopatiwa
msamaha huo ni wale wagonjwa wenye magonjwa ya kifua kikuu, UKIMWI na Saratani
ambao wako kwenye Hatua ya mwisho (terminal stage).
Pia, wengine
waliopata msamaha huo ni wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini au zaidi,
wafungwa wa kike walioingia gerezani wakiwa na ujauzito, pamoja na walioingia
gerezani na watoto wanaonyonya na wasio nyonya.
Aidha wafungwa
wenye ulemavu wa akili wametakiwa kuthibitishwa na jopo la waganga chini ya
Mwenyekiti ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa au Mganga Mkuu wa Wilaya.
Hata hivyo, Msamaha
huo hautawahusisha wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa au kwa makosa ya kujaribu
kuwaua wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa na adhabu hiyo kubadilishwa
kuwa kifungo cha maisha au kifungo gerezani, wafungwa wanaotumikia kifungo
gerezani, wafungwa wanaotuhumiwa na makosa ya kujihusisha na usafirishaji na
matumizi ya dawa za kulevya kama vile Cocain, Heroin na Bangi.
Wafungwa elfu tatu
mia tatu kumi na tisa watafaidika na msamaha huo ambapo mia tano themanini na
tano wanaachiliwa huru leo, huku wafungwa elfu
mbili mia saba thelathini
na nne watabaki gerezani kumalizia
sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya msamaha huo.
Mategemeo ya
serikali ni kuwa wafungwa hao watarejea katika jamii na kushirikiana na
wanajamii katika ujenzi wa taifa na
watajiepusha na kutenda makosa ili wasirejee gerezani.
MAGUFULI AWAACHIA HURU ZAIDI YA WAFUNGWA 3000.
Reviewed by safina radio
on
April 26, 2018
Rating:
No comments