MKUU WA MKOA WA GEITA MHANDISI ROBERT GABRIEL AZITAKA HALMASHAURI ZA MKOA HUO KUSIMAMIA NA KUWATAMBUA WACHIMBAJI WADOGO.


Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robart Gabriel amezitaka halmashauri za Mkoa huo kusimamia na kuwatambua wachimbaji wadogo wa madini wote walioko kwenye Halmashauri zao.


Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita Mhandisi Gabriel amesema kuwa wachimbaji wengi bado hawatambuliki serikalini, hivyo kushindwa kupata kodi stahiki kutoka kwa wachimbaji hao.

Akizungumza kwa niaba ya madiwani wa halmashauri hiyo ya Geita Diwani Jeremiah Ikangala amesema kuwa tatizo la kutokusanywa kwa mapato katika eneo la madini wamelibaini na tayari wamelichukulia hatua suala hilo.

Aidha baadhi ya watu waliokuwepo katika Mkutano huo wameunga mkono tamko la Mkuu wa mkoa huyo na kusema kuwa jitihada kubwa zinastahili kuwekwa katika usimamizi wa shughuli za uchimbaji wa madini kwa kuwa kuna mapato mengi yanayotakiwa kulipwa serikalini.

MKUU WA MKOA WA GEITA MHANDISI ROBERT GABRIEL AZITAKA HALMASHAURI ZA MKOA HUO KUSIMAMIA NA KUWATAMBUA WACHIMBAJI WADOGO. MKUU WA MKOA WA GEITA MHANDISI ROBERT GABRIEL AZITAKA HALMASHAURI ZA MKOA HUO KUSIMAMIA NA KUWATAMBUA WACHIMBAJI WADOGO. Reviewed by safina radio on April 26, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.