MAWAZIRI WA ELIMU AFRIKA WATAKUTANA KUJADILI MAENDELEO ENDELEVU KUHUSU ELIMU KWA BARA LA AFRIKA.


Mawaziri wa elimu kutoka nchi za Afrika wiki ijayo watafanya mkutano wa siku tatu mjini Nairobi, nchini Kenya ili kutathmini hadhi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu kuhusu elimu katika bara hilo.

Image result for Shirika la Elimu na Sayansi la Umoja wa Mataifa (UNESCO)

Mkutano huo ulioandaliwa na Shirika la Elimu na Sayansi la Umoja wa Mataifa (UNESCO) pamoja na Umoja wa Afrika, utawakutanisha mawaziri wa elimu kutoka Afrika, watunga sera na washauri kutoka sekta ya umma na binafsi kuhusu suala la elimu.

Image result for Umoja wa Afrika

 UNESCO imesema wajumbe pia watajadili, kuongeza uelewa na kubadilishiana maoni kuhusu jinsi ya kuunganisha Malengo Endelevu ya Maendeleo na Mkakati wa Elimu kwa bara la Afrika katika kuboresha mifumo ya ajenda, sheria ya elimu, sera, mipango, ufadhili, usimamizi na mawasiliano.

MAWAZIRI WA ELIMU AFRIKA WATAKUTANA KUJADILI MAENDELEO ENDELEVU KUHUSU ELIMU KWA BARA LA AFRIKA. MAWAZIRI WA ELIMU AFRIKA WATAKUTANA KUJADILI MAENDELEO ENDELEVU KUHUSU ELIMU KWA BARA LA AFRIKA. Reviewed by safina radio on April 18, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.