ILI KUKABILIANA NA WIZI WA KIMTANDAO SERIKALI YAJIWEKEA MIKAKATI MBALIMBALI.
Naibu waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Mh
Atashasta Nditiye amesema kuwa ili kukabilina na wizi wa kimtandao hapa nchini
serikali imejiwekea mikakati mbalimbali ikiwemo kuwatumia wataalamu wake wa
ndani wa TEHAMA ili kujadiliana namna ya kumaliza wizi huo.
Mh Nditiye ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma
wakati akijibu swali la mbunge wa Busekelo Mh Wilfred Mwakibete aliyetaka kujua
serikali imejiwekea mikakati gani ili kupambana na wizi wa kimtandao
unaoendelea hapa nchini.
Amesema kuwa ni kweli wizi wa kimtandao unaendelea
hapa nchini na kwa kutambua hilo serikali itakaa na wataalamu wa TEHAMA ili
kutengeneza progmu maalumu itakayosaidia kuzuia uhalifu wa kimtandao.
Ameongeza kuwa mbali na serikali kukutana na
wataalamu hao imepanga pia kwenda kujifunza kwa nchi ambazo zimefanikiwa
kupambana na uhalifu wa kimtandao ikiwemo nchi za Israel,India na Marekani ili
kujua ni njia gani walizotumia kupambana na uhalifu huo.
Bunge la bajeti linaendelea mjini Dodoma ambapo
wabunge wanaendelea kujadili bajeti ya wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiliano
kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 iliyowasilishwa hapo jan na waziri wa wizara
hiyo Mh Makame Mbarawa.
ILI KUKABILIANA NA WIZI WA KIMTANDAO SERIKALI YAJIWEKEA MIKAKATI MBALIMBALI.
Reviewed by safina radio
on
April 24, 2018
Rating:
No comments