SERIKALI INA MPANGO WA KUIMARISHA MINARA YA SIMU ILIYOKO MIPAKANI.
Naibu waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Mh
Atashanta Nditiye amesema kuwa serikali ina mpango wa kuimarisha minara ya simu
iliyopo mipakani ili kuzuia mwingiliano wa mawasiliano kati ya nchi na nchi.
Mh Nditiye ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma
wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Vunjo Mh James Mbatia aliyetaka
kujua serikali ina mpango gani wa kuzuia mwingiliano wa mawasiliano ya simu kwa
wananchi walioko katika maeneo ya Vunjo na Rombo mkoani Kilimanjaro.
Amesema kuwa maeneo mengi yaliyoko mipakani hapa
nchini yanakabiliwa na mwingiliano wa mawasiliano ya simu kutoka nchi jirani na
ili kukabiliana na changamoto hiyo serikali kupitia mfuko wa fursa kwa wote wa
mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA itaimarisha minara iliyoko katika mipaka
hiyo ili kumaliza tatizo hilo.
Hata hivyo bunge la 11 mkutano wa 11 linaendelea
Jijini Dodoma ambapo wabunge wanaendelea kujadili bajeti kuu ya serikali kwa
mwaka wa fedha wa 2018/219.
SERIKALI INA MPANGO WA KUIMARISHA MINARA YA SIMU ILIYOKO MIPAKANI.
Reviewed by safina radio
on
April 27, 2018
Rating:
No comments