JMEC YASEMA KUWA TAREHE MPYA YA MAZUNGUMZO YA AMANI SUDANI KUSINI ITATANGAZWA NA MWENYEKITI WA IGAD.
Wafuatiliaji
wa amani nchini Sudan Kusini wamesema kuwa mazungumzo yajayo ya amani
yaliyopangwa kufanyika tarehe 26 Aprili mwaka huu yameahirishwa hadi taarifa itakapotolewa.
Tume ya
Ufuatiliaji na Tathmini JMEC imesema kuwa tarehe mpya ya mazungumzo hayo
itatangazwa na mwenyekiti wa baraza la mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo ya
Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki IGAD.
Hata
hivyo kwa mujibu wa habari zilizotolewa ,Tume hiyo inasema kuwa kuahirishwa kwa
kwa mazungumzo hayo kutatoa nafasi ya mazungumzo yenye ufanisi kwa wadau
mbalimbali wanaohusika na masuala hayo ya amani.
JMEC YASEMA KUWA TAREHE MPYA YA MAZUNGUMZO YA AMANI SUDANI KUSINI ITATANGAZWA NA MWENYEKITI WA IGAD.
Reviewed by safina radio
on
April 18, 2018
Rating:
No comments