SHIRIKA LA NDEGE LA ETHIOPIA KUENEZA SHUGHULI ZAKE NCHINI CHINA.
Shirika
la Ndege la Ethiopia limesema lina nia ya kueneza soko lake nchini China na
kuwa shirika la ndege la kirafiki kati ya China na Afrika.
Hayo
yamesemwa kwenye ripoti ya Shirika hilo iliyowasilishwa kwenye bunge la nchi
hiyo, ambayo pia imesema zaidi ya raia 4,000 wa China wanapanda ndege yao kila
siku.
Mkuu
wa ofisi ya huduma za kimataifa ya Shirika hilo Bw. Esayas Woldemariam amasema
Shirika hilo limechukua hatua kadhaa ili kuwavutia wageni wa China, ikiwemo
kituo cha kuuliza maswali kwa Kichina na wahudumu wa China wanaotoa huduma ya
chakula cha kichina.
SHIRIKA LA NDEGE LA ETHIOPIA KUENEZA SHUGHULI ZAKE NCHINI CHINA.
Reviewed by safina radio
on
April 19, 2018
Rating:
No comments