UTOAJI WA MAFUNZO CHANJO YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KUSAIDIA KUFUTA UPOTOSHAJI.
Wanahabari Mkoani Njombe wamesema kuwa utoaji wa
mafunzo ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa watoto wa umri wa miaka
14 utasaidia kufuta upotoshaji wa lengo la utoaji wa chanjo hiyo kwa jamii.
WANAHABARI WA MKOA WA NJOMBE |
Wakizungunza mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo baadhi
ya wamahabari wamesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia wanahabari kusahihisha mitazamo
tofauti iliyopo kwenye jamii na lengo la chanjo hali inayosababisha watoto
wengine kukosa chanjo hiyo.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk.
Buni Mwamasage amewataka wanahabari hao kufuata weledi wao kutoa elimu ya
kutosha kwa jamii ili kufanikisha azma ya serikali ya kuzuia maambukizi ya saratani
ya kizazi kwa miaka ya baadae.
Aidha, amesema kuwa kutokana na utafiti wa kisayansi
kumebainika kuwa umri wa miaka 14 ni mzuri katika kuzuia maambukizi ya ugonjwa
huo kwa kuwa wasichana katika umri huo hawajajihusisha na tendo la ndoa huku
akibainisha kuwa huduma ya chanjo hiyo itatolewa katika vituo vya serikali na
vituo vya mashirika ya kijamii.
Saratani ya Mlango wa Kizazi imekuwa tishio kwa nchi
zinazoendelea ikiwemo Tanzania ambapo takwimu zinaonesha kuwa takribani watu elfu
hamsini hupoteza maisha kila mwaka hapa nchi kutokana na ugonjwa huo.
UTOAJI WA MAFUNZO CHANJO YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KUSAIDIA KUFUTA UPOTOSHAJI.
Reviewed by safina radio
on
April 23, 2018
Rating:
No comments