WHITE HOUSE YASEMA UTAWALA WA TRUMP UMEFANYA MAZUNGUMZO NA KOREA KASKAZINI.
Ikulu ya Marekani
White house imesema kuwa utawala wa Rais Donald Trump umefanya mazungumzo ya
ngazi ya juu na Korea Kaskazini, ingawa hakujakuwepo mawasiliano ya moja kwa
moja kati ya Rais Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un.
Gazeti la Washington
Post limeripoti kuwa mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani CIA Mike Pompeo
alifanya safari ya siri mjini Pyongyang wiki ya kwanza ya mwezi Aprili mwaka
huu na kukutana na Kim.
Vyanzo vyenye taarifa
kuhusu ziara hiyo, vimenukuliwa na gazeti hilo, vikieleza kuwa mazungumzo hayo
yamelenga juu ya maandalizi ya mkutano wa kilele baina ya Trump na Kim
unaotarajiwa kufanyika siku chache zijazo.
Mazungumzo ya ngazi
ya juu kati ya nchi hizo mbili pia yamethibitishwa na Rais Trump katika mkutano
na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe katika jimbo la Florida.
Trump amesema
anaridhia majadiliano ya kumaliza rasmi vita vya Korea.
WHITE HOUSE YASEMA UTAWALA WA TRUMP UMEFANYA MAZUNGUMZO NA KOREA KASKAZINI.
Reviewed by safina radio
on
April 18, 2018
Rating:
No comments