UJERUMANI NA IRAQ KUSHIRIKIANA KUWARUDISHA NYUMBANI WAKIMBIZI
Waziri wa maendeleo
wa Ujerumani Gerd Müller amesema nchi yake na Iraq zitashirikiana katika
kutekeleza zoezi la kuwarudisha nyumbani wakimbizi wa Iraq.
GERD MULLER |
Waziri Müller amesema
wakimbizi elfu kumi wa Iraq walioko nchini Ujerumani watasaidiwa ili waweze
kurudi kwao,ambapo amesema Ujerumani na
Iraq zimekuabliana kushirikiana kwa undani zaidi ili kuwasaidia kurudi nyumbani
Wairaki wanaoomba hifadhi ya ukimbizi nchini Ujerumani.
Waziri huyo wa
maendeleo wa Ujerumani aliyefanya ziara nchini Iraq pia amesema Ujerumani na
Iraq zitafanya kazi kwa pamoja ili kuwapa fursa za elimu na ajira Wairaki
wanaorejea nchini kwao.
Hata hivyo Kati ya
wairaki elfu ishirini na nne wanaoishi nchini Ujerumani kwa sasa,12,000
hawajafanikiwa kupata hifadhi ya ukimbizi.
UJERUMANI NA IRAQ KUSHIRIKIANA KUWARUDISHA NYUMBANI WAKIMBIZI
Reviewed by safina radio
on
April 23, 2018
Rating:
No comments