WATU 10 WAMEFARIKI NCHINI CANADA
Watu kumi wamepoteza maisha baada ya mwanaume mmoja aliyekuwa
akiendesha gari kugonga umati wa watu katika jiji la Toronto nchini
Canada,tukio ambalo polisi imeliita shambulizi la makusudi.
![]() |
GARI LILILOUA WATU |
Kisa hicho kimetokea jana katika eneo lenye umbali wa kilomita
16 kutoka ukumbi wa mkutano wa mawaziri wa mataifa makubwa kiviwanda G7.
Mkuu wa polisi katika jiji hilo Mark Saunders amethibitisha
idadi ya vifo na kusema shambulizi hilo lilikuwa la makusudi lakini tukio hilo
halihusiani na mkutano huo.
Waziri wa usalama wa Canada Ralph Goodale amewaambia waandishi
wa habari kwamba ni mapema kusema tukio hilo ni la kigaidi.
Kumekuwa
na matukio ya magari makubwa kutumiwa na magaidi na kusababisha
vifo katika maeneo yenye mikusanyiko
WATU 10 WAMEFARIKI NCHINI CANADA
Reviewed by safina radio
on
April 24, 2018
Rating:
No comments