WANANCHI WOTE WANAOISHI MABONDENI NCHINI WATAKIWA KUONDOKA.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh
Majaliwa Kasim Majaliwa amewataka wananchi wote waishio mabondeni kote nchini
kuondoka mara moja ili kuepukana na majanga yanayotokana na mvua zinazoendelea
kunyesha.
WAZIRI MKUU MAJALIWA. |
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa maagizo hayo leo bungeni
mjini Dodoma wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu ambapo
amesema kuwa maafa yaliyo sababishwa na mafuriko ya maji ya mvua ni makubwa kwani hadi sasa wako waliopoteza
maisha na wengine nyumba zao kusombwa na maji.
Aidha Mh Majaliwa amesema kuwa yapo maeneo ya
bondeni ambayo yameathiriwa na mvua huku shughuli za uokozi zikiwa ni
changamoto kutokana na maeneo hayo kutokupitika kwa urahisi kutokana na
miundombinu mibovu iliyopo.
Amesema kuwa pamoja na madhara makubwa yanayotokana
na mvua tayari serikali kupitia wizara ya ofisi ya makamu wa rais muungano na
mazingira pamoja na ofisi ya rais TAMISEMI imeandaa miradi ya kuboresha
miundombinu ya barabara na mifereji ya kusafirisha maji katika mikoani ikiwemo
jiji la Dar-es-salaam.
Hata hivyo amewataka wabunge kutoingiza suala la
siasa katika zoezi hilo la wananchi kuondoka mabondeni bali wawahamasishe
kuhama kwa kuwa serikali inaandaa fedha ya kuboresha miundombinu katika maeneo yote ya mabondeni ili maji yaweze kupi
ta kwa urahisi na kuepukana na majanga ya mvua.
WANANCHI WOTE WANAOISHI MABONDENI NCHINI WATAKIWA KUONDOKA.
Reviewed by safina radio
on
April 19, 2018
Rating:
No comments