MITI ELFU MBILI MIA TANO IMEPANDWA KATIKA MSITU WA CHOME SHENGENA
Ili kuzua uharibifu wa mazangira katika msitu wa
Chome Shengena ulioko katika wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro serikali imepanda
miti elfu mbili mia tano katika msitu huo kati ya mwaka wa 2012 hadi 2017.
Hayo yameelezwa leo bungeni mjini Dodoma na naibu
waziri wa nchini ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira Mh Kangi Lugola wakati
akijibu swali la mbunge wa Same Mashariki Mh Nangejwa Kaboyoka aliyetaka kujua
serikali ina mpango gani wa kuzuia uharibifu wa mazingira unaoendelea kufanywa
katika msitu wa Chome Shengena.
Mh Lugola amesema kuwa msitu huo umekuwa ukiharibiwa
na wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo pamoja na
uchimbaji wa madini ambapo ili kuhakikisha mazingira ya msitu huo yanarudi
katika hali yake ya kawaida serikali iliamua kupanda miti hiyo na kugawa miti
mingine ya asili.
Ameongeza kuwa mbali na kupandwa kwa miti hiyo
serikali pia imeweka ulinzi katika msitu huo ili kuzuia shughuli za kibinadamu ambapo
ulinzi huo unafanywa na askari kutoka jeshi la kujenga taifa (JKT).
Hata hivyo naibu waziri huyo amewataka viongozi wote
waliopewa mamlaka kote nchini kusimamia sheria na taratibu zilizowekwa za
utunzaji wa mazingira hapa nchini.
MITI ELFU MBILI MIA TANO IMEPANDWA KATIKA MSITU WA CHOME SHENGENA
Reviewed by safina radio
on
April 25, 2018
Rating:
No comments