VIJANA WATAKIWA KUFANYA KAZI BADALA YA KUKAA VIJIWENI
Vijana Mkoani Iringa wametakiwa kufanya kazi kwa
bidii na kuondokana na tabia ya kukaa vijiweni ili kuunga mkono juhudi za Rais
Dk. John Magufuli za kupambana kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda kwa
faida ya wananchi wote.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Amina
Masenza wakati wa Tamasha lililoandaliwa na baadhi ya wasanii wa filamu ambao
wako mkoani Iringa kwaajili ya kutoa elimu kwa vijana kuachana na tabia ya kutumia
muda mwingi vijiweni.
Aidha, Masenza amesema kuwa Mkoa wa Iringa utajengwa
na wanairinga endapo watajituma na kufanyakazi ili kuufanya mkoa huo kuwa mkoa
wa viwanda.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya Iringa Bw Richard
Kasesela amesema kuwa watapambana kuhakikisha kuwa wanazidi kuwapa elimu vijana
ili wahamasike kufanya kazi.
Hata hivyo, zaidi ya wasanii sitini wako mkoani
Iringa kutoa elimu kwa vijana mbali mbali kuachana na tabia ya kukaa vijiweni
ambapo kaulimbiu yao ni amka kijana tujenge nchi yetu.
VIJANA WATAKIWA KUFANYA KAZI BADALA YA KUKAA VIJIWENI
Reviewed by safina radio
on
April 16, 2018
Rating:
No comments