ZIMBABWE KUSHIRIKI MKUTANO WA JUMUIYA YA MADOLA.


Zimbabwe itashiriki katika Mkutano wa viongozi wa nchi kutoka muungano wa Jumuiya ya Madola unaofanyika wiki hii jijini London nchini Uingereza.

Image result for PICHA YA EMMERSON MNANGAGWA
RAIS WA ZIMBZBWE EMMERSON MNANGAGWA

Itakuwa mara ya kwanza kwa Zimbabwe kurejea katika mkutano huo baada ya kufungiwa mwaka 2003 kwa sababu ya wizi wa kura na ukiukwaji wa haki za binadamu chini ya uongozi wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Robert Mugabe.

Zimbabwe haijaalikuwa kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola tangu nchi hiyo kuzuiliwa kwa vikao vyote vya jumuiya hiyo tangu mwaka 2003 kufuatia matokeo ya uchaguzi wa rais, mnamo mwezi Machi mwaka 2002.

Kadhalika Muungano wa Ulaya ulitangaza vikwazo dhidi ya nchi hiyo. 

Kwa mujibu wa makisio ya wachunguzi wa kimataifa, wakati huo Mugabe alishinda kwa matumizi ya mabavu, vitisho dhidi ya upinzani na ulaghai katika uchaguzi.

ZIMBABWE KUSHIRIKI MKUTANO WA JUMUIYA YA MADOLA. ZIMBABWE KUSHIRIKI MKUTANO  WA JUMUIYA YA MADOLA. Reviewed by safina radio on April 17, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.