TAKUKURU MKOANI KILIMANJARO YAKAMILISHA UCHUNGUZI WA TUHUMA DHIDI YA KIWANDA CHA KUKOBOA KAHAWA.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU
mkoani Kilimanjaro imekamilisha uchunguzi wa tuhuma dhidi ya kiwanda cha
kukoboa kahawa cha Tanganyika Coffee Cawe On TCCO.
Akizungumza mkoani humo Kaimu Mkuu wa TAKUKURU wa mkoa
huo Bw Mosess Obuda amesema kuwa tayari mafaili sita yamesha wasilishwa kwa
mkurugenzi wa Mashtaka kwa ajili ya kuyaombea kibali cha kuwapeleka watuhumiwa
mahakamani.
Aidha amesema kuwa muda sio mrefu taasisi hiyo
itapata majibu ambayo taasisi na wananchi wanatarajia kuwa haki ya wananchi wa
Moshi na wanachama wa vyama vya ushirika ambapo kitu kikubwa ni mali za
wanachama wa ushirika huku akisema kuwa moja ya malalamiko yaliyofanyiwa
uchunguzi ni ubadhirifu wa fedha za manunuzi ya mashine mpya.
Hata hivyo ameongeza kuwa TAKUKURU bado inaendelea
kuwatafuta washtakiwa wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai ambao ni aliyekuwa
Afisa Utumishi Faraja Ndatu na Afisa Uchumi Isaya Bayege kwa tuhuma za Kughushi
vitambulisho na kujipatia mkopo wa fedha shilingi milioni thelathini na tano
kutoka Benki ya CRDB.
Naye Afisa Mkuu wa TAKUKURU Mkoani humo Benedict Mongela
amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu wameokoa fedha shilingi milioni tisa
ambazo zilikuwa hazijatolewa risiti.
Hata hivyo, mwaka 2016 Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa Mkoani Kilimanjaro ilipokea malalmiko ya uwepo wa
ubadhirifu wa fedha katika kiwanda hicho.
TAKUKURU MKOANI KILIMANJARO YAKAMILISHA UCHUNGUZI WA TUHUMA DHIDI YA KIWANDA CHA KUKOBOA KAHAWA.
Reviewed by safina radio
on
April 13, 2018
Rating:
No comments